SUZA Selected Applicants 2018 – 2019 Certificate and Diploma

By | November 29, 2018

SUZA Selected Applicants 2018 – 2019 Certificate and Diploma

Utangulizi Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kilitangaza kupokea maombi ya udahili kwa kozi zake tofauti za cheti na diploma katika dirisha la kwanza la udahili kwa mwaka wa masomo 2018-2019 tarehe 20/07/2018. Baada ya kufunga dirisha la wali la udahili, chuo kimefanya upembuzi wa maombi yote kwa mujibu wa vigezo vilivyoainishwa na kwa mujibu wa uwezo wa kirasilimali wa chuo wa kuendesha kozi hizo. Yafuatayo ni ni majina yaliyothibitishwa kwa udahili wa kozi hizo husika kwa dirisha la udahili la awali.

Angalizo:

1. Waombaji wote ambao majina yao hayakuorodheshwa wafahamu kuwa inaweza kuwa:

i. Kozi walizoomba zilikuwa na ushindani mkubwa na hivyo, kutokana na uchache wa nafasi hawakuweza kuchaguliwa. Sababu hii zaidi inagusa kozi za afya zote isipokuwa ya “Diploma in Environmental Health Sciences”, ambayo bado haijajaa na maombi bado yanapokelewa.

ii. Sifa za muombaji zilikuwa hazitoshelezi kwa mujibu wa vigezo.

iii. Au sababu yoyote ya kiufundi iliyotokezea wakati wa kujaza fomu ya maombi “online”, ikapelekea muombaji kutokamilisha fomu yake ya maombi na hivyo kutozingatiwa katika upembuzi.

2. Waliofanikiwa kuchaguliwa, taarifa za hatua inayofuata itatumwa kupitia akaunti zao walizotumia wakati wa kujaza fomu za maombi.

3. Waombaji waliokuwa hawakuchaguliwa na wanahisi walikuwa na sifa za kutosheleza, wanaombwa wafike kwa Maafisa udahili waliopo katika kampasi zote za SUZA kwa kupata maelekezo na kurekebishiwa kasoro zao.

4. Waombaji ambao wanahusika na sababu (1(i)) hapo juu, wanashauriwa kuomba kozi nyengine ambazo watazipendelea kwa mujibu wa sifa zao. Waombaji hawa hawatahusika na malipo ya maombi; yaani chuo kitazingatia malipo yao waliyofanya awali.

5. Kwa waombaji wapya, wanatakiwa kufuata taratibu zote za maombi, ikiwemo malipo. 6. Maombi ya kozi za Cheti na Diploma yanaendelewa kupokelewa katika dirisha hili la pili la udahili hadi tarehe 20/09/2018.

Download State University Zanzibar SUZA Selected Applicants / Candidates 2018 – 2019 Certificate / Diploma

See Also

2018 – 2019 Selected Applicants / Candidates for Public University Colleges in Tanzania

2018 – 2019 Selected Applicants / Candidates for Private University Colleges in Tanzania

See also